Kiswahili - Form III

Jisajili na kozi ya Kiswahili Form III ya TESEA Academy kwa kufuata mtaala mpya wa NECTA. Pata masomo ya sarufi, fasihi, uandishi, na maandalizi bora ya mitihan...

0

... English
... Certificate Course
... 0 Students
... 00h 00m

Course Overview

Kozi ya Kiswahili Form III ya TESEA Academy imeandaliwa kwa kuzingatia mtaala mpya wa NECTA ili kumsaidia mwanafunzi kuelewa kwa kina dhana muhimu za Kiswahili, kukuza uwezo wa kuandika kwa usahihi, na kujenga uelewa mpana wa sarufi, fasihi, matumizi ya lugha, na uandishi wa kitaaluma.


Hii ni kozi iliyolenga kumwezesha mwanafunzi wa kidato cha tatu kuwa na msingi imara wa Kiswahili kwa maandalizi ya Kidato cha Nne na mitihani ya NECTA kwa ujumla. Tunafundisha kwa njia ya kisasa, rahisi, na inayompa mwanafunzi uwezo wa kujifunza kwa haraka na kwa ufanisi.


Baada ya kumaliza kozi hii, mwanafunzi ataweza:


  • Kutumia Kiswahili sanifu kwa mawasiliano ya kuzungumza na kuandika.

  • Kuchambua na kutumia vipengele vya sarufi kwa usahihi.

  • Kuelewa na kufasiri maana ya matini (comprehension) kwa umakini.

  • Kuandika insha za aina mbalimbali kwa kufuata vigezo vya NECTA.

  • Kuchambua kazi za fasihi kwa kutumia mbinu sahihi.

  • Kujibu maswali ya mtihani kwa ufanisi kwa kutumia mbinu za ufahamu na mazoezi ya mara kwa mara.


Kozi ya Form III Kiswahili imegawanyika katika maeneo makuu yanayofuata:


1. Sarufi na Matumizi ya Lugha

Hapa mwanafunzi atajifunza matumizi sahihi ya lugha kwa mujibu wa kanuni za Kiswahili. Mada hujumuisha:

  • Aina za maneno na uhusiano wake katika sentensi

  • Uundaji wa sentensi sahihi

  • Matumizi ya viwakilishi, vivumishi, vielezi, viunganishi n.k.

  • Nyakati, kauli na viambishi

  • Makosa ya kawaida ya sarufi na jinsi ya kuyaepuka


    2. Ufahamu (Comprehension Skills)

Sehemu hii inamjengea mwanafunzi uwezo wa:

  • Kusoma matini na kutoa hoja muhimu

  • Kutambua dhamira, wazo kuu na wazo msaidizi

  • Kujibu maswali ya ufahamu kwa kutumia ushahidi kutoka kwenye matini

  • Kupanua msamiati na matumizi ya maneno katika muktadha


3. Uandishi (Writing Skills)

Uandishi ni sehemu muhimu ya NECTA. Kozi hii inakuwezesha:

  • Kuandika insha za hoja, wasifu, simulizi na insha za maelezo

  • Kutumia utangulizi, kiini na hitimisho kwa ufanisi

  • Kutumia lugha fasaha na mfuatano wa mawazo

  • Kuandika barua rasmi na isiyo rasmi (kulingana na mtaala)

  • Kuandika hotuba, tangazo, risala au kumbukumbu (kulingana na mtaala mpya)


4. Fasihi na Uchambuzi wa Kazi za Fasihi

TESEA Academy inatoa ufundishaji wa fasihi kwa njia rahisi na yenye kueleweka:

  • Aina za fasihi simulizi na andishi

  • Vipengele vya tamthilia, ushairi na riwaya

  • Dhamira, wahusika, mtindo na ujumbe

  • Uchambuzi wa maswali ya fasihi kwa mtazamo wa NECTA


Kozi hii imeundwa kwa mtindo unaomweka mwanafunzi katika mazingira ya kujifunza kwa ufanisi:


✅ Video/maelezo mafupi yaliyo na mifano
✅ Maswali ya mada kwa mada (topic-based questions)
✅ Mitihani ya mazoezi (mock style) kwa viwango vya NECTA
✅ Majibu na uchambuzi wa kina
✅ Mbinu za kujibu maswali kwa alama nyingi
✅ Kurejea mada ngumu kwa urahisi kupitia mifano halisi


Kozi hii inafaa kwa:


  • Wanafunzi wa Form III wanaotaka kuimarisha Kiswahili

  • Wanafunzi wanaotaka kujenga msingi wa Form IV NECTA

  • Wanafunzi wenye changamoto ya sarufi na uandishi

  • Wale wanaotaka kupata alama za juu kwa mazoezi na mbinu sahihi

  • Walimu au wazazi wanaotaka nyenzo bora za kujifunzia

See More

Course curriculum

Course curriculum Empty

Requirment

Outcomes

Instructor

...
TESEA Teacher

0.0

  • ... 6 Students
  • ... 71 Courses
  • ... 0 Review

View Details

Reviews

Rate this course :

Remove all
...

Free

... Enroll Now
  • ...

    Students

    0
  • ...

    language

    English
  • ...

    Duration

    00h 00m
  • Level

    form-III
  • ...

    Expiry period

    Lifetime
  • ...

    Certificate

    Yes
Share :